Responsive image
Responsive image
Posted : October 06, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP- Simon Sirro
Responsive image

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP- Simon Sirro amewataka wanasiasa kuacha kuingilia majukumu ya Jeshi la Polisi juu ya upelelezi wa watuhumiwa wa shambulizi la Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo mkoani Njombe kufuatia kuwepo kwa baadhi ya wabunge kukosoa kauli yake aliyoitoa akiwa mkoani Mtwara ya kumtaka dereva wa Mbunge huyo kuripoti kwa ajili ya kutoa taarifa ya tukio hilo.

 IGP Simon Sirro akatoa rai kwa wanasiasa kuacha kuingilia majukumu ya jeshi hilo, hususani katika masuala ya upelelezi wa matukio ya uhalifu.

Kuhusu upelelezi juu ya tukio la kujeruhiwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, IGP Sirro amesema jeshi hilo linaendelea na upelelezi ili kupata ushahidi unajitosheleza na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa hizo.

Katika hatua nyingiena IGP Sirro amesema njia pekee ya kumaliza mauaji yanayohusishwa na imani za ushirikina ni kutoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari na nyumba za ibada.

Mkoani Njombe kumekuwa kukiripotiwa matukio mbalimbali ya kihalifu ya mauaji yanayohusishwa na imani za kishirikina, visasi na ubakaji.

 

TATU ABDALLAH 

OCTOBA 06, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment