Responsive image
Responsive image
Posted : September 22, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Kikosi cha wataalamu wa jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ kikikagua mipaka ya eneo la machimbo ya madini ya Tanzanite, Mererani ili kuanza ujenzi wa uzio kuzunguka eneo hili kama mheshimiwa Rais Dkt. JOHN MAGUFULI alivyoagiza.
Responsive image

Siku moja baada ya agizo la Rais Dkt. JOHN MAGUFULI  kwa  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania - JWTZ kujenga uzio kuzunguka machimbo ya madini ya tanzanite eneo la Mererani, kikosi cha wataalamu wa Jeshi hilo kimeanza kukagua mipaka ya eneo hilo ili kuanza ujenzi.

 

Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Michael Isamuyo amewaomba wananchi katika maeneo yatakayopitiwa na ujenzi huo pamoja na wamiliki wa migodi kutoa ushirikiano.

 

Ukaguzi huo umefanyika angani na ardhini kuzunguka machimbo ya tanzanite yaliyopo Mererani mkoani Manyara.

 

Mara bada ya kutembelea eneo hilo, Meja Jenerali ISAMUYO amesema wataanza kazi hiyo mara moja kama walivyoagizwa na Amri Jeshi Mkuu Rais John Magufuli.

 

Zoezi hili limeungwa mkono na  wachimbaji wa madini katika eneo hili  wakielezea kuleta manufaa kwao na taifa.

 

 

SECHELELA KONGOLA

SEPTEMBA 22, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment