Responsive image
Responsive image
Posted : September 21, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John akizindua barabara ya KIA-Mererani yenye urefu wa kilometa 26
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli ameliagiza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania -JWTZ kujenga uzio wa ukuta kuzunguka eneo lote la machimbo ya madini ya Tanzanite ya bloku A hadi D ili kuzuia wizi wa madini hayo na kunufaisha wananchi wa eneo la Mererani mkoani Manyara.

Akizungumza katika eneo la Mererani wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wakati wa uzinduzi wa barabara ya KIA-Mererani yenye urefu wa kilometa 26, Rais Dkt. Magufuli amesema hatua hiyo itaiwezesha serikali kupata fedha na mwekezaji bila udanganyifu wowote.

Rais Magufuli ameagiza wawekezaji waliokuwa wanashikiliwa kwa ajili ya kutoa maelezo waachiwe ili kutoa ushirikiano kwa tume ya kujadili madini chini ya Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi.

Rais Magufuli yuko mkoani Arusha ambapo Jumamosi Sept 23 mwaka huu atawatunuku kamisheni maafisa wanafunzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania –JWTZ.

 

Sechelela Kongola

21 Septemba 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment