Responsive image
Responsive image
Posted : September 19, 2017 (8 months ago) By TBC
Responsive image
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya, Wafula Chebukati
Responsive image

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya imeviita vyama viwili vikuu nchini Kenya vyenye wagombea kiti cha Urais katika uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 17 mwezi ujao katika meza ya mazungumzo ili kuangalia uwezekano wa kubadili tarehe ya uchaguzi.

Msukumo wa kuibadili tarehe hiyo umetokana na taarifa kutoka Kampuni ya SAFRON MOFFAN ya UFARANSA iliyopewa kandarasi ya kupeperusha matokeo ya kura kwa njia ya Kielektroniki kusema kuwa haitakuwa tayari kuifanya kazi hiyo tarehe 17 mwezi ujao.

Kampuni hiyo imesema kazi hiyo inachukua muda mrefu kutengeneza mfumo maalum wa Kieletroniki unaojulikana kama soft-wea kwa ajili ya kutekeleza jukumu hilo.

Kufuatia kikwazo hicho cha kiufundi Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya, Wafula Chebukati amevitaka Vyama vya JUBILEE na Muungano wa Upinzani wa NASA kuhudhuria mkutano huo hapo kesho bila ya kukosa ili waweze kukubaliana juu ya tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo wa marudio.

Wakati hayo yakiendelea viongozi wa NASA wameituhumu Kampuni ya Safron Moffan kwa kupokea hongo kutoka maafisa wa serikali ya Rais Uhuru Kenyatta ili kuruhusu mfumo wa kusafirisha matokeo ya kura kwa njia ya Kielectronik kupunguza kura za mgombea wa Nasa Raila Odinga.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment