Responsive image
Responsive image
Posted : May 19, 2017 (11 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa Balozi Augustine Mahiga
Responsive image

Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki limependekeza  kuondolewa vikwazo vya biashara ili kuwezesha wananchi wa mataifa ya Afrika Mashariki kunufaika na fursa zilizopo.

Akizungumza nje ya mkutano wa baraza hilo ulilofanyika Jijini Dar es salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa Balozi Augustine Mahiga amesema mkutano huo utatoa ripoti kuhusu makubaliano hayo kwa viongozi  ili maeneo yote yaliyojadiliwa yafanyiwe kazi.

Aidha mkutano huo pia unapendekeza kuwa nchi ambazo zina fursa nzuri za kilimo ikiwemo Tanzania na Uganda zitumie fursa hiyo kuzalisha mazao kama mahindi na mchele ambayo yatauzwa katika nchi wanachama hivyo kukuza mchangamano wa kibiashara.

Mapendekezo hayo yatajadiliwa katika mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki watakaokutana Jijini Dar es salaam  Tarehe 20 mwezi huu.

Katika mkutano huo Rais John Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anatarajiwa kukabidhi Uenyekiti kwa Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

 

 

DOMINICK MOKIWA

MEI 19, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment