Responsive image
Responsive image
Posted : May 19, 2017 (11 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu
Responsive image

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu ameiambia Marekani kumuondoa balozi wake nchini Syria kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa Kikurdi nchini humo -YPG.

Mevlut amesema ni wazi kuwa Balozi wa Marekani, Brett Mcgurk wa Muungano wa mapambano dhidi ya Kundi la IS amekuwa akiyaunga mkono makundi ya YPG na PKK.

Aidha Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ameunga mkono kauli ya waziri wake akiongeza kuwa Uturuki itashambulia iwapo itashuhudia uvamizi wa Kundi la Kikurdi nchini Syria.

Mvutano kati ya Uturuki na Marekani umeendelea baada ya Uturuki kuwazuia wabunge 250 kuingia nchini humo.

Ujerumani imetishia kuwaondoa wanajeshi wake kutokana na hatua ya Uturuki na Waziri Mevlut amesema Ujerumani inaweza kuwaondoa wanajeshi wake

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment