Responsive image
Responsive image
Posted : May 19, 2017 (11 months ago) By TBC
Responsive image
Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys
Responsive image

Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua ya nusu fainali ya michuano ya vijana ya afrika inayoendelea huko nchini Gabon baada ya kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya timu ya taifa ya vijana ya Angola katika mchezo wake wa pili wa kundi B.

Magoli ya Serengeti Boys katika mchezo huo yamefungwa na Kevin Naftal katika dakika ya 6 na Abdallah Selemani katika dakika ya 69 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Yohana Mkomola huku lile la kufutia machozi kwa Angola likufungwa na Melo katika dakika ya 18.

Matokeo hayo yanaipa nafasi Serengeti Boys kuongoza kundi B kwa kufikisha alama nne huku wakisaliwa na mchezo mmoja wa kuhitimisha hatua ya makundi dhidi ya Niger utakaofanyika May 21 huko kwenye visiwa vya Port Gentil

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment