Responsive image
Responsive image
Posted : April 26, 2017 (10 months ago) By TBC
Responsive image
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini- TANTRADE Christopher Chiza
Responsive image

Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini- TANTRADE- imewashauri wadau wa ngozi kuchakata ngozi nchini ili kuziongezea thamani  badala ya kuzisafirisha nje zikiwa ghafi.

 Akizungumza na washiriki wa semina ya siku tatu kuhusiana na fursa zinazopatikana katika bidhaa za ngozi Mwenyekiti wa Bodi hiyo Christopher Chiza amesema kusafirisha ngozi ghafi ni sawa kutoa ajira kwa watu wa mataifa mengine. 

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTANTRADE Edwin Rutageruka amesema semina hiyo inalenga  kuongeza ujuzi wa wadau wa bidhaa za ngozi nchini ili kuongeza ajira na ufanisi hasa kwa vijana.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment