Responsive image
Responsive image
Posted : April 22, 2017 (10 months ago) By TBC
Responsive image
Utafiti wa kilimo wapelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao kwa wakulima
Responsive image

Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mazao ya kilimo ya IITA imesema teknolojia walizoanzisha za kutafiti wadudu waalibifu na aina mpya ya mbegu zimepelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya muhugo, soya , kunde na migomba hapa nchini.

Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwao, mtafiti wa mifumo ya uzalishaji wa kilimo Dkt. Frederick Baijukya amesema wameweza kufanya utafiti wa mbegu bora na dawa ya kuua wadudu waharibifu kulikongeza uzalishaji kwa wakulima wa mikoa ya kaskazini na kanda ya ziwa.

Aidha mtafiti wa maabara wa IITA James Legg amesema Tanzania inapata hasara ya dola milioni hamsini kwa magonjwa ya mimea kila mwaka hivyo IITA imefanya utafiti wa magonja ya mihogo ya batobato na michirizi ya kaawia ili kuwapunguzia gharama

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment