Responsive image
Responsive image
Posted : April 21, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
mwili wa Dkt. Elly Macha kuagwa
Responsive image

Waziri Mkuu  Majaliwa ameongoza Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuuaga mwili wa Mbunge wa Viti Maalum kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA, Dkt. Elly Macha.

Wakati wa shughuli hiyo ya kuaga mwili wa Dkt.  Macha, viongozi pamoja na wabunge mbalimbali wametoa salamu zao za  rambirambi na kumuelezea kuwa alikua ni Mbunge aliyejitolea katika kuhakikisha haki za watu wenye ulemavu zinapatikana.

Baada ya kukamilika kwa shughuli ya kuaga, Mwili wa Dakta umesafirishwa kwenda Mkoani Arusha ambapo hapo kesho utasafirishwa kwenda Kirua Vunjo Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko.

Dakta Elly Macha alifariki dunia nchini Uingereza tarehe 31 mwezi uliopita alipokua akipatiwa matibabu.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment