Responsive image
Responsive image
Posted : April 21, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
wananchi wa Arusha watakiwa kutotoa mwanya wa kurubuniwa katika rushwa
Responsive image

Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa -TAKUKURU Mkoa wa Arusha imewaonya watumishi  wenye tabia ya kutengeneza mazingira ya rushwa  wakati wa utoaji  huduma kuacha tabia hiyo kwani hudhoofisha ufanisi  na upatikanaji  wa huduma kwa wananchi.

Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo mkoa wa Arusha, Frida  Wikesi ametoa tahadhari hiyo alipokutana na waandishi wa habari jijini Arusha, kutoa taarifa ya utendaji wao wa kipindi cha Julai 2016 hadi Machi 2017 ambapo  amesema wananchi wamekuwa wakifikisha malalamiko yao TAKUKURU, hivyo ni vema watumishi wakawahudumia wananchi  kwa uadilifu.

Aidha viongozi hao wamewataka wananchi kutotoa mwanya wa kurubuniwa katika rushwa ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa wanapodaiwa au kuona matukio ya rushwa pamoja na kutoa ushirikiano wa ushahidi pindi wanapohitajika ili kutokomeza vitendo hivyo.

 

 

SECHELELA KONGOLA

APRILI 21, 2017 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment