Responsive image
Responsive image
Posted : April 21, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick
Responsive image

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick ametoa muda wa siku 14 kwa Halmashauri ya wilaya ya Moshi kuvunja bodi ya Jumuiya ya watumia maji katika mradi wa Maji wa Korini kutokana na bodi hiyo kushindwa kusimamia mradi huo.

Sadick ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi huo na kubaini uwepo wa tofauti za kisiasa baina ya wajumbe wa bodi hiyo zinazosababisha mradi kukosa usimamizi tangu uzinduliwe  Agosti mwaka 2014.

Mhandisi wa Maji wilaya ya Moshi, Injinia Elidhili Mrutu amesema tofauti hizo zimechangia wananchi kutumia huduma ya maji bila kuchangia huku usimamizi wa mradi ukikosekana

Mradi wa maji wa Korini unahudumia wakazi wa vijiji vya Korini Juu, Korini Kati na Korini Kusini katika Kata ya Mbokomu wilayani Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro umegharimu kiasi cha shilingi Bilioni moja na Milioni 314.

 

 

 SAUDA SHIMBO

APRILI 21, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment