Responsive image
Responsive image
Posted : April 21, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Tumbaku ni moja ya zao la biashara linaloweza kuinua hali ya uchumi wa wananchi Tanzania
Responsive image

Wakulima  na wadau wa zao la Tumbaku toka katika mikoa mbalimbali nchini wamepongeza serikali kwa hatua inazochukua dhidi ya viongozi wa vyama vya ushirika wanaohujumu zao hilo.

Wakizungumza katika mkutano wa wadau wa zao la tumbaku waliokutana mkoani Singida kufanya tathimni ya zao hilo kwa mwaka  2016/17 wamesema hatua hizo zitasaidia kupunguza ubadhirifu wa fedha za wakulima unaofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika vinavyonunua na kuuza zao hilo.

Katika taarifa yake Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Tumbaku Tanzania Stanley Mnozya amesema atahakikisha wanasimamia maagizo ya serikali na taratibu za ununuzi wa zao hilo katika msimu huu wa ununuzi.

 Naye, Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amesisitiza matumizi ya mashine za kielektoniki katika ununuzi wa zao hilo

 

 LEONARD  MANGA

APRILI 21, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment