Responsive image
Responsive image
Posted : April 21, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Bonde la Mto Ruaha Mkuu
Responsive image

Baadhi ya watendaji wa halmashauri za Manispaa ya Iringa na wilaya hiyo wamesema kuwa chanzo cha kushindwa kusimamia sheria za hifadhi ya mazingira ni muingiliano wa masuala ya siasa wakati wa utekelezaji wa sheria hizo.

Watendaji hao wametoa kauli hiyo mbele ya wajumbe wa Kikosi kazi cha kuokoa Ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu kilichozinduliwa hivi karibuni na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Watendaji hao wamekiri kuwa vyanzo vya maji vinavyotiririsha maji kwenye Mto Ruaha Mkuu vimegubikwa na shughuli za ufugaji na kilimo hadi ndani ya vyanzo.
Wamesema wamekuwa wakijaribu mara kadhaa kuwaondoa wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji lakini wanakwamishwa na masuala ya kisiasa

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment