Responsive image
Responsive image
Posted : April 21, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Maporomoko ya udongo yaua Colombia
Responsive image

Watu kadhaa wamekufa nchini Colombia baada ya nchi hiyo kukumbwa na maporomoko mengine ya udongo.

Mwezi uliopita nchi ya Colombia ilikumbwa na mapromoko mabaya zaidi ya udongo kuwahi kutokea nchini humo yaliyoambatana na mvua za msimu na kusababisha vifo vya zaidi ya watu mia tatu.

Serikali ya Colombia ilidhamiria kufanya uchunguzi ili kuthibitisha taarifa kuwa uharibifu wa mazingira ndio chanzo cha maporomoko ya udongo.

Nchi hiyo ilishuhudia kingo za mito mingi zikipasuka na milima kugeuka kuwa matope yaliyofukia makazi ya watu

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment