Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Rais Magufuli afanya mazungumzo na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini –TUCT
Responsive image

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa serikali itaendeleza kuimarisha zaidi ushirikiano kati yake na wafanyakazi kwa manufaa ya taifa na kwamba ipo tayari kupokea maoni na ushauri utakaotolewa na vyama vya wafanyakazi wenye lengo la kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Ikulu Jijini Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini –TUCTA.

Aidha Rais Magufuli amewaeleza viongozi hao kuwa serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi na itaendelea kuchukua hatua za kukabiliana nazo kama ambavyo imeanza kufanya.

Kwa upande wao viongozi wa TUCTA wakiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo Tumaini Nyamhokya wamempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa zinazofanywa na serikali katika kujenga uchumi imara, kuimarisha utendaji kazi wa watumishi wa serikali, kupambana na rushwa, kuondoa watumishi hewa na kulipa madeni ya watumishi.

Viongozi hao wameahidi kushirikiana na serikali katika kusimamia haki na wajibu wa wafanyakazi na wameomba serikali iendelee kufanyia kazi masuala mbalimbali ya wafanyakazi ikiwemo kuwalipa stahili zao na kuboresha mazingira ya kazi

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment