Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa maonesho ya mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi
Responsive image

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kutoa huduma ya mikopo bila ya mazingira ya rushwa ili watanzania wengi waweze kunufaika na mikopo hiyo.

Akifungua maonesho ya mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi- NEEC- Mjini Dodoma, waziri mkuu ameitaka mifuko hiyo kujenga nidhamu na kutoa huduma ya mikopo kwa waombaji kwa weledi na masharti nafuu.

Akitoa taarifa ya mifuko hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi NEEC, Being’i Issa amesema serikali inamifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi 19 yenye jumla ya mtaji wa shilingi tirioni tatu na imewafikia wananchi milioni moja

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment