Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (11 months ago) By TBC
Responsive image
Ruto aliyejiunga na NASA
Responsive image

Muungano wa upinzani nchini Kenya -NASA umesema utamtangaza atakayeshikilia bendera yake ya Urais mnamo tarehe 27 mwezi huu.

Akizungumza katika mkutano wa kumpokea Gavana wa Kaunti ya Bomet, Isack Ruto aliyejiunga na muungano huo Seneta wa Kaunti ya Bungoma, Moses Wetangula amesema kiongozi huyo atatajwa katika mkutano utakaofanyika Uwanja wa Uhuru Park Jijini Nairobi.

Wetangula amesema tayari viongozi hao ambao wamekuwa wakikutana kwa takriban siku tatu zilizopita wamepiga hatua ya kumchagua mmoja wao kuongoza muungano huo.

Viongozi Wakuu wa Muungano wa NASA ni aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga wa Chama cha ODM, aliyekuwa Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka wa Chama cha Wiper, Moses Wetangula wa Chama cha Ford Kenya na Issack Ruto wa Chama cha Mashinani.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment