Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (a week ago) By TBC
Responsive image
Maboresho yaliyofanywa na bandari ya Dar es salaam yarudisha wateja
Responsive image

Maboresho yaliyofanywa na bandari ya Dar es salaam yamemrudisha mteja mkubwa wa kutoka Zambia kampuni ya MM Intergrated Steel Mills baada ya kuamua kupitisha shehena ya mizigo yake tani laki moja na ishirini elfu na kuachana na bandari ya Mombasa nchini Kenya aliyokuwa akiitumia

Akizungumza wakati wa kupokea maloli 14 yenye shehena ya mitambo ya migodini inayokwenda Zambia, Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini TPA Deusdedit Kakoko amesema mteja huyo amerejea baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa bandari ya Dar es salaam SM.

Kwa upande wake wakala wa mizigo wa kampuni hiyo Azim Dewij amesema MM Intergrated Steel Mills itakuwa inapitisha tani elfu nne hadi elfu kumi za mizigo kila mwezi katika bandari ya Dar es salaam

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment