Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
wakazi wa Zanzibar
Responsive image

Meya wa manispaa ya mjini Unguja Khatib Abdulrahiman Khatib amewashauri Wafanyabiashara visiwani Zanzibar kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha za mikopo kwa kuziwekeza katika miradi ili kukuza mitaji ya biashara zao.

Akizungumza kwenye mafunzo ya siku moja ya usimamizi wa fedha yaliyoandaliwa na benki ya NMB mjini Unguja na kuwashirikisha  wafanyabiashara 200 , Khatib amesema usimamizi na nidhani ya matumizi ya fedha yatawawezesha wafanyabiashara kuboresha biashara zao na kukuza mtaji.

Wakizungumzia mafunzo hayo, mfanyabiashara wa utalii Biabwa Abdala Mohamed na mfanyabiahara wa huduma ya elimu Ameir Hassan Ameir wamasema mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kukuza biashara zao maradufu

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment