Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Responsive image

Mshindi wa medali ya fedha katika mchezo wa kuruka juu kwenye  michuano ya olimpiki ya mwaka 2008 huko jijin Beijing, China Mwingereza Germaine Mason amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 34 kwa ajali ya pikipiki, nchini Jamaica .

 Mason ambaye ana asili ya Jamaica, alibadilisha uraia mwaka 2006 na kuanza  kuiwakilisha Uingereza katika mashindano mbalimbali , alishinda medali ya fedha katika michuano  ya Olimpiki huko Beijing mwaka 2008 akishika nafasi ya pili nyuma ya Mrussia Andrey Silnov.

 Kupitia ukurasa wake wa Twitter Waziri Mkuu wa Jamaica, Andrew Holness amesema rambirambi za serikali ya Jamaica ni kwa ndugu na wana michezo wote

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment