Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Responsive image

Mchezaji tenis namba mbili kwenye viwango vya ubora wa tenesi kwa kina dada, Serena Williams atakosa michuano yote iliyosalia kwa msimu huu kwa kuwa yu mjamzito.

Taarifa hizi zinakuja wiki 12 tu tangu alipoandikisha rekodi ya kutwaa taji kubwa (Grand Slam) la 23 tangu aanze kucheza mchezo huo na anatarijiwa kujifungua majira ya kipupwe.

Taarifa iliyonukuliwa kwenye mtandao wake wa snapchat ikisindikizwa na ujumbe unaosomeka kuwa ana ujauzito wa majuma 20 ilithibitishwa na muwakilishi wa mchezaji huyo na hivyo kumfanya akose michuano iliyosalia ambayo ingempasa ashiriki.

Hata hivyo mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 35 amekuwa nje ya uwanja tangu alipotwaa ubingwa wa Australian Open mjini Melbourne kwa kile kilichoelezwa kuwa anasumbuliwa na majeraha ya goti

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment