Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Chelsea na Spurs vinara
Responsive image

Vilabu za Chelsea na Tottenham Hotspurs vimetawala kwenye kikosi cha wachezaji 11 bora wa Ligi kuu England msimu huu ambacho kimetangazwa na Chama cha Wachezaji Soka la Kulipwa nchini humo, ambapo timu hizo mbili zina wachezaji wanne kila moja katika kikosi hicho.

Mabeki Gary Cahill na David Luiz pamoja na viungo wa kati N'golo Kante na Eden Hazard ndio wachezaji wa Chelsea waliojumuishwa kwenye kikosi hicho.

Huku Tottenham ikiwa na walinzi wa pembeni Kyle Walker na Danny Rose, kiungo wa kati Dele Alli na mshambuliaji Harry Kane.

Mlinda lango wa Manchester United, David De Gea, Sadio Mane wa Liverpool na mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku pia wamo kwenye kikosi hicho.

Washambuliaji wawili Zlatan Ibrahimovic wa Manchester United na Alex`s Sanchez wa Arsenal wamekosa nafasi kwenye kikosi hicho bora cha wachezaji 11 kwa msimu wa 2016-2017 licha ya kuwemo kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwenye ligi hiyo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment