Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Mohamed Fakhi
Responsive image

Sakata linalosumbua hivi sasa kwenye soka la Tanzania kuhusu kadi tatu za njano zinazomuhusu mlinzi wa kati wa timu ya Kagera Sugar Mohamed Fakhi limeshindwa kuamuliwa hii leo na hatimae kazi hiyo ameachiwa mwenyekiti wa kamati ya Katiba, sheria na hadhi ya Wachezaji Richard Sinamtwa.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ameimbia TBC kuwa tayari kamati hiyo imeshakamilisha kila kitu ila kwa sasa mwenyekiti huyo anaandika hukumu na hivi karibuni ataitangaza. 

Kamati hiyo imekutana kwa kipindi cha siku tatu na  sasa kinachosubiliwa na wengi ni kuwekwa wazi kwa majibu ya  kamati hiyo ili kuweza kujua ukweli wa jambo hilo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment