Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Responsive image

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania kuiamini serikali wakati ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa matukio mbalimbali ya uhalifu ambayo yamekua yakitokea katika baadhi ya maeneo nchini  na kuzusha hofu miongoni mwa wakazi wa maeneo hayo.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa wito huo Bungeni Mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

Kuhusu ombi lililotolewa bungeni la kuitaka serikali kuomba msaada mataifa nje ili kuchunguza matukio mbalimbali yanayotokea nchini  likiwemo lile la watu kupotea, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa serikali ina uwezo na vyanzo vyake vya namna ya kubaini na kudhibiti matukio kama hayo.

Kikao cha leo cha bunge kilianza kwa kuapishwa  kwa Mbunge wa Viti Maalumu   Getrude Lwakatare.

 

 

BAKARI MWARABU

APRILI 20, 2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment