Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
Responsive image

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA - Charles Kichere ahakikishe anaweka utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara mara kwa mara kama njia ya kujadili na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara hao.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Kichere kuhusu namna bora ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara nchini kama hatua ya kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi wa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kusikitishwa na baadhi ya Maafisa wa TRA kuwanyanyasa wafanyabiashara na wengine kuwabambikizia kodi kubwa hali ambayo inazua malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kama TRA itafanya mabadiliko yeyote ya ulipaji wa kodi ikawafahamisha wafanyabiashara hao mapema ili kuondoa usumbufu mkubwa unaoweza kutokea katika ulipaji wa kodi pindi wanapoagiza bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi.

Makamu wa Rais pia ameipongeza TRA kwa kazi kubwa inayoifanya katika ukusanyaji wa mapato na amewapa moyo wa kuongeza bidii katika ukusanyaji wa kodi hizo ambazo Serikali inatumia katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini.

 Kwa upande wake, Kamishna Kichere amemuahidi Makamu wa Rais kuwa atafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha malalamiko mbalimbali yanayotolewa na Wafanyabiashara yanapata ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment