Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Afya, Maendeleo, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
Responsive image

Serikali imetangaza kuwachukulia hatua za kisheria Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini watakaoshindwa kudhibiti vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua  kwa kuwa vifo hivyo vinaweza kuzuilika iwapo kutakuwa na mipango madhubuti katika kila halmashauri.

Tangazo hilo la serikali limetolewa Jijini Dar es salaam  na Waziri wa Afya, Maendeleo, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kando ya mkutano wa Chama cha Madaktari Bingwa wa Uzazi na Magonjwa ya Wanawake Tanzania – AGOTA.

Zaidi ya asilimia sitini ya wajawazito nchini wamekua wakijifungulia katika vituo vya Afya na asilimia nyingine iliyobaki bado wanajifungulia majumbani hususani maeneo ya vijijini.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment