Responsive image
Responsive image
Posted : August 03, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli alipokuwa akizungumza na wananchi eneo la Mkata wilayani Handeni Mkoani Tanga
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli amealiagiza Jeshi la kujenga taifa JKT Kambi ya Mgambo iliyopo tarafa ya Mzundu  Wilayani Handeni Mkoani Tanga kurudisha eneo la ekari 50 walilochukua kwa wananchi baada ya kushindwa kuliendeleza kwa kipindi cha miaka saba.

 

Rais Dkt. Magufuli ameagiza kurudishwa eneo hilo hii leo wakati akisalimia wananchi wa eneo la Mkata akiwa njiani kuelekea Jijini Tanga baada ya kupata malalamiko kwamba jeshi hilo lilichukua eneo la ardhi na kushindwa kuliendeleza huku wananchi wakikosa maeneo ya kufanyia shughuli zao.

 

Aidha Rais Dkt. Magufuli amewataka vijana nchini wasitumike kuiharibu amani ya nchi na kuwataka kufanya kazi kwa bidiii.

 

Rais Dkt. John Magufuli yupo ziarani Mkoani Tanga ambapo siku ya Jumamosi yeye pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wataweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Mkoani Tanga ambapo zaidi ya watu elfu 15 watapata ajira katika ujenzi huo. 

 

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Handeni umesimama ili kupisha uchunguzi wa matumizi ya fedha za ujenzi milioni 500 zilizopelekwa kutekeleza kazi hiyo kwa awamu ya kwanza.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment