Responsive image
Responsive image
Posted : August 03, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Aliyekuwa bingwa wa dunia katika ndondi Wladmir Klitschko
Responsive image

Aliyekuwa bingwa wa dunia katika ndondi Wladmir Klitschko amestaafu katika ndondi na hivyo kufuta  uwezekano wowote wa mechi ya marudiano dhidi ya Anthony Joshua.

 

Raia huyo wa Ukraine mwenye umri wa miaka 41 alipigwa knockout katika raundi ya 11 na bingwa wa sasa Joshua katika uwanja wa Wembley mnamo mwezi Aprili .

 

Joshua mwenye umri wa miaka 27 alitarajia Klitschko atashiriki mechi ya marudiano mjini Las Vegas tarehe 11 mwezi Novemba  mwaka huu.

 

Klitschko ambaye ni bingwa mara mbili wa uzani mzito duniani anastaafu  akiwa ameshinda mara 64 na kushindwa mara 5.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment