Responsive image
Responsive image
Posted : July 31, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Tanzania na Uganda zasaini hati ya makubaliano ya kupeleka umeme kwenye Vijiji vya Mpakani mwa nchi hizo ​
Responsive image

​Serikali za Tanzania na Uganda zimetiliana saini Mkataba wa Makubaliano ya Awali (MoU) wa kupeleka umeme kwenye Vijiji vya Mpakani mwa nchi hizo.​

Hati ya Makubaliano hayo ilisainiwa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akiwakilisha Wizara ya Nishati na Madini (Tanzania) na Waziri wa Nishati wa Uganda, Dk. Simon D’Ujanga, wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa nchi hizo kuhusu ushirikiano kwenye masuala ya mpakani, uliofanyika mjini Bukoba, wilayani Kagera.

Makubaliano ya msingi katika Hati iliyosainiwa ni utekelezaji wa Mradi wa kupeleka umeme kwenye vijiji vya Nangoma, katika eneo lililopo mpakani mwa Tanzania na Uganda na vijiji vingine vya maeneo hayo kwa kutokea upande wa Tanzania.

Akifafanua zaidi kuhusu makubaliano husika, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, ambaye pia alishiriki Mkutano huo mkubwa, alisema kuwa Wakala wa Nishati Vijijini kwa upande wa Tanzania (REA-Tanzania) utahusika katika kugharamia ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 33 kufikisha umeme katika eneo la mpakani, umbali wa kilomita 0.8 kwa gharama ya Dola za Marekani 36,923.05.

 

31/7/2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment