Responsive image
Responsive image
Posted : July 31, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Raphael Daudi anakuwa mchezaji wa nane mpya kusajiliwa na Yanga
Responsive image

Kiungo huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia timu hiyo ya mtaa wa Jangawani na Twiga.

Kiungo huyo Raphael Daudi anakuwa mchezaji wa nane mpya kusajiliwa na Yanga katika dirisha hili la kiangazi la usajili hadi sasa, baada ya makipa Mcameroon Youth Rostand kutoka African Lyon iliyoshuka Daraja, kipa wa timu ya Serengeti Boys Ramadhan Kabwili, Mlinzi Abdallah Hajji  maarufu kwa jina la Ninja kutoka timu ya  Taifa Jang’ombe ya Zanzibar, viungo Pius Buswita kutoka Mbao FC, Papy Kabamba Tshishimbi, Mkongo kutoka Mbabane Swallows ya Swaziland, Hussein Akilimali ambae ni mchezaji huru na mshambuliaji Ibraahim Hajib kutoka Simba.

Katika hatua nyingine zikiwa zimesalia siku sita zoezi la usajili kwa njia ya mtandao (TMS) kwa timu za ligi kuu, ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili bado ni la kusuasua ambao taarifa zinasema hadi hadi sasa jumamosi jioni takriban wachezaji 114 majina yao yalikuwa yameingizwa kwenye mtandao huo wa TMS kati ya wachezaji 1600 wanaotakwa kusajiliwa na timu zote 64 za madaraja hayo matatu huku timu ya Yanga ikiwa inaongoza ikiwa imesajili wachezaji 22.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment