Responsive image
Responsive image
Posted : July 31, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Kumekuwa na sintofahamu miongoni mwa wanachama wa simba kufuatia nia ya mfanyabiashara Mohamed Dewji kutaka kuwekeza katika clabu hiyo
Responsive image

Baraza la wadhamini la klabu ya Simba limesisitiza kuwa klabu ya Simba  haiwezi kumilikiwa na mtu mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Simba , Katibu mkuu wa baraza Mzee Hamis Kilomoni amesema suala la klabu ya Simba kumilikiwa na mtu mmoja hilo haliwezekani kamwe.

Kumekuwa na sintofahamu kubwa miongoni mwa wanachama , wa klabu ya Simba tangu mfanyabiashara Mohamed Dewji ambaye ni mwanachama na mdau mkubwa wa klabu hiyo  atangaze nia ya kutaka kuwekeza hisa asilimia 51 katika klabu hiyo zikiwa na thamani ya shillingi billioni 20.

Suala hilo limesababisha mpasuko mkubwa ndani ya klabu ya Simba ambapo baadhi ya wanachama wanaunga mkono mabadiliko ya uwekezaji  huku wengine wakipinga  mabadiliko hayo .

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI
Ladies FashionShabiki namba moja  |  7 months ago   |   July 31, 2017
"Hii ni timu ya wananchi haitapendeza kumilikiwa na mtu mmoja"

Leave Your Comment