Responsive image
Responsive image
Posted : July 28, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Rais wa shirikisho la riadha Tanzania Antony Mtaka
Responsive image

Wachezaji wa timu ya taifa ya riadha itakayokwenda kushiriki mashindano ya olympic London  Uingereza   mwezi ujao  itaagwa  julai 31,mwaka huu katika hotel ya Kempiski  jijini Dar es salaam.

Rais wa shirikisho la riadha Tanzania Antony Mtaka amesema timu hiyo inaendelea vyema na maandalizi yake . Mtaka  amesema mwaka huu Tanzania imejiandaa vizuri kwani inapeleka wachezaji  wanane (8) wakiongozwa na

mwanariadha mzoefu ,Alphonce Simbu na kwamba  anatarajia  kuwa timu hiyo itapeperusha vema bendera ya taifa.

Aidha Mtaka amesema maandalizi ya  timu hiyo ni mazuri licha ya kwamba  kuna ushindani mkubwa na nchi nyingine ambapo amewaomba  watanzania wawaombee wachezaji hao ili waweze kurudi na medali lukuki .

 Ameongeza kuwa wachezaji hao wana sifa za ushiriki na kwamba  maandalizi yaliyofanywa na makocha wao ni ya kutosha hivyo wanatarajia kupata ushindi.

 

Pascal Michael                  

 28/7/207

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI
Ladies FashionPongwa masiku  |  7 months ago   |   July 31, 2017
"Tunaomba walete medali ha ya shaba sio ya na story tumeshazichoka"

Leave Your Comment