Responsive image
Responsive image
Posted : July 25, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Mama Salma Kikwete
Responsive image

Balozi wa lugha ya kiswahili  Afrika mashariki Mama Salma Kikwete  amesema  lugha ya kiswahili inazidi kukua katika nchi za Afrika Mashariki kihistoria na kusema faida ya kuzungmza hii inazidi kuonekana .

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Kamusi Kuu ya Kiswahili​ uliofanyika leo jijini NAIROBI ambapo ameeleza kuwa juhudi kubwa za kuimarisha lugha ya kiswahili imefanyika katika nchi zote za Afrika Mashariki.

Mama Salma ameipongeza kampuni ya Longhorn Publishers na BAKITA kwa kazi ya  kutunga Kamusi Kuu ya Kiswahili na kuiwezesha kupata ithibati ya taasisi zinazosimamia elimu katika nchi zetu mbili za  Kenya na Tanzania.

Amesema Ithibati hiyo ni ushahidi wa kukubalika kwa  kamusi hii kwa matumizi rasmi  katika nchi hizi mbili.

 

Angella  Msangi 

25/7/2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment