Responsive image
Responsive image
Posted : July 22, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Rais John Magufuli
Responsive image

Rais John Magufuli amewahakikishia wakazi wa mkoa wa  Kigoma kuwa serikali itahakikisha inashughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili zikiwemo za miundombinu ya barabara maji pamoja na umeme.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akiwahutubia wakazi wa wilaya za Kakonko, Kibondo na Kasulu wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi la ujenzi wa barabara za Kibondo - Nyakanazi na  Kasulu – Kidahwe.

Akiwa njiani mkoani Kigoma Rais Dkt, John Magufuli amelazimika kusimamisha msafara wake  mara kadhaa kuzungumza na wananchi waliofurika barabarani kumpokea huku akiendelea kusisitiza masuala mbali mbali likiwemo linalohusu wakimbizi waliopo mkoani Kigoma..

Rais magufuli anaendelea na ziara yake mkoani kigoma ikiwa ni ziara ya kwanza kuifanya katika mkoa huo toka aingie madarakani mwaka 2015.

 

 

EGIDIUS AUDAX

JULAI 22,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment