Responsive image
Responsive image
Posted : July 17, 2017 (10 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
Responsive image

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri na Waganga wakuu wa mikoa na wilaya zote chini kuhakikisha kunakuwa Dawa za kutosha muda wote katika maeneo yao.

Waziri Ummy Mwalimu ametoa agizo hilo wilayani Lushoto mkoani Tanga wakati akikagua maendeleo ya Ujenzi wa Ghala la kuhifadhi Dawa katika Hospitali ya Wilaya hiyo na kueleza kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo.

Mkakati wa Serikali ni kuhakikisha Dawa na vifaa Tiba vya kutosha vinakuwepo wakati wote katika Hospitali, Zahanati na Vituo vyote vya afya ili kuwawezesha  wakazi wa maeneo mbalimbali nchini kupata huduma bora za afya.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, - Martine Shigela amesema  kuwa Wilaya  Nne kati ya Nane za Mkoa huo tayari zimemaliza ujenzi wa Maghala ya kuhifadhi Dawa.

 

Nora Uledi

Julai 17,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment