Responsive image
Responsive image
Posted : July 15, 2017 (10 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akisikiliza wananchi wenye matatizo na kero za ardhi
Responsive image

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amekesha ofisini kwake pamoja na wananchi takribani 189 wenye Matatizo na Kero za ardhi.

Waziri Lukuvi ametumia takriban saa 20 kusikiliza kero za wananchi ambao waligoma kuondoka ofisini kwake hadi kero zao zitakapopatiwa ufumbuzi Kazi ambayo ilianza  majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 9 usiku.

Hata hivyo wananchi walilazimika kulala Wizarani wakisubiri kuonana na Waziri kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya watu.

Wananchi wengi wenye matatizo na Kero za ardhi kutoka maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga, Kibiti na Dar Es Salaam kwa ujumla wametumia fursa hiyo ya kipekee ya kuonana na Waziri mwenye dhamana ya Ardhi na kumuelezea kero zao na hatimaye kupatiwa ufumbuzi papo hapo.

Wananchi hao wamesifu hatua hiyo ya Waziri Lukuvi kukutana nao ana kwa ana na kuzitatua kero zao za ardhi kwa kuwa haijawahi kutokea.

 

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment