Responsive image
Responsive image
Posted : July 15, 2017 (10 months ago) By TBC
Responsive image
Naibu waziri wa Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla
Responsive image

Naibu waziri wa Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tunduru kuhakikisha anaboresha huduma za Afya katika kituo cha Afya  Mkasale ambacho kimebainika kuwa na huduma mbovu huku kikiwa na uchakavu kwenye majengo  yake hali.

Dkt. Kigwangalla ameutaka Uongozi wa Halmashahuri ya Tunduru kushughulikia suala hilo ndani ya miezi mitatu ikiwemo Mkandarasi wa Maji kuhakikisha anaingiza mifumo ya maji ndani ya kituo hicho.

Aidha ametaka uongozi wa  kijiji kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira yanayozunguka kituo hicho cha Mkasale kutokana na mazingira yake kutoridhisha.

Waziri Kigwangalla amesema lengo la serikali ya awamu ya tano ni kupunguza kwa asilimia kubwa changamoto zinazozikabili wilaya ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vya kinamama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

 

Nora Uledi

Julai 15,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment