Responsive image
Responsive image
Posted : July 15, 2017 (8 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki
Responsive image

Nchi ya Uturuki leo inaadhimisha mwaka mmoja tangu kushindwa kwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi lililofanywa na baadhi ya askari ambapo watu mia mbili sitini walikufa na wengine elfu mbili mia moja tisini na sita walijeruhiwa.

Taarifa zaidi kutoka nchini humo zinaarifu kuwa maadhimisho hayo yanafanyika katika miji mbalimbali nchini humo ambapo Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ataungana na mamia ya wananchi katika viunga vya jiji la Istanbul kuadhimisha siku hiyo ambapo baadhi ya askari walishindwa jaribio la  kuipindua serikali yake.

 

Ramadhan Mpenda

Julai 15,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment