Responsive image
Responsive image
Posted : July 14, 2017 (10 months ago) By TBC
Responsive image
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba
Responsive image

Mamlaka ya Mawasiliano Nchini -TCRA imezitoza faini kampuni sita za simu za mikononi shilingi Bilioni 11.2 kwa kukiuka utaratibu wa kusajili namba za simu au laini na kulirudia kosa hilo kwa mara ya pili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amezitaja kampuni hizo za simu kuwa ni Airtel Tanzania, Smart, Tigo, Vodacom, Zantel na Halotel.

Amesema kampuni hizo zinatakiwa kulipa fedha hizo kabla ya tarehe 14 mwezi Oktoba mwaka huu.

Kilaba amesema baada ya kuchunguza ukiukwaji huo wa taratibu za usajili wa wateja wamekutwa na makosa matano ambayo yanahatarisha usalama wa nchi.

 

Stanley Ganzel

14 Julai 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI
Ladies FashionPongwa  |  8 months ago   |   September 08, 2017
"Unajua hii mitandao ya simu inaponzwa na wakala wao wajaribu kubadirisha mfumo. Hao wachina walizani Tanzania dampo ya kuzoa madini warudi makwao."

Leave Your Comment