Responsive image
Responsive image
Posted : July 12, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam , Paul Makonda.
Responsive image

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam , Paul Makonda ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la kisasa la huduma za dharura katika Hospitali ya Temeke ambalo ujenzi wake utagharimu zaidi ya Shilingi Million 800 linalofadhiliwa na Ubalozi wa Japan hapa nchini.

 

Akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe hilo Makonda amesema jengo hilo litakuwa na uwezo wa kusaidia zaidi ya watu 2000 kwa siku ambapo litakuwa na chumba cha upasuaji, chumba cha wagonjwa mahututi, vyumba vya uangalizi maalumu wa wagonjwa pamoja na vyumba vya madaktari na kusema kuwa hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali katka kuboresha sekta ya afya.

 

Aidha jengo hilo litakuwa na vyumba maalumu vya watoto njiti, ambapo lengo ni kuhakikisha mgonjwa yeyote wa dharura anapatiwa huduma ya haraka na kupunguza ya mkusanyiko wa wagonjwa wa dharura katika Hospital ya Taifa Muhimbili.

 

Kwa upande Mwakilishi wa Balozi wa Japan nchini Hiroyuki Kubota amesema Serikali ya Japan itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment