Responsive image
Responsive image
Posted : July 12, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Mama Advera Kyaruzi ambaye awali alidhulumiwa kiasi cha shilingi milioni 10 kabla ya kurudishiwa baada ya Rais Dkt. John Magufuli kuingilia kati.
Responsive image

Mkazi mmoja wa Kata ya Mto Wa Mbu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, Mama Advera Kyaruzi amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli baada ya kurudishiwa Shilingi Milioni 10 alizodhulumiwa na mfanyabiashara mmoja baada ya kumuuzia mchele.

 

Akizungumza na TBC Jijini Arusha, Advera Kyaruzi amesema alifikia uamuzi wa kwenda Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi Siku ya Mei Mosi kumuona Rais Magufuli baada ya kukosa msaada katika ngazi mbalimbali na Rais kumuagiza Mkuu wa Mkoa wa ARUSHA kushughulikia suala hilo.

 

Kyaruzi amesema aliamua kutafuta haki yake kwa kumuona Rais John Magufuli kutokana na nyumba yake kutishiwa kuuzwa pamoja na kufunguliwa kesi ya kudaiwa fedha ambazo alikopa.

 

 Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema viongozi, wapo kwa ajili ya kuhudumia wananchi wanyonge wamekuwa wakidhulumiwa mali zao.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI
Ladies FashionMAGAMBO WANGA  |  9 months ago   |   July 16, 2017
"KWA HILI RAIS AJUWE KUNA WATU WENGI WANAONYANYASWA NA VIONGOZI WETU ANGETOA KWALIPIO KWA VIONGOZI WANAO WADHARAU WATU WA CHINI"

Leave Your Comment