Responsive image
Responsive image
Posted : July 12, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea ujenzi wa daraja la mto Lukuledi lenye urefu wa Mita 30 linalounganisha mikoa ya Lindi na Mtwara.
Responsive image

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  ameelezea kuridhishwa mradi wa ujenzi wa daraja la mto Lukuledi lenye urefu wa Mita 30 linalounganisha mikoa ya LINDI na Mtwara.

 

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea ujenzi huo utakaogharimu Shilingi Bilioni 5 Nukta 4  na kusema kuwa daraja hilo ni mkombozi kwa Wakazi wa mikoa hiyo miwili  hasa wa wilaya za RUANGWA na Masasi.

 

Waziri Mkuu  Majaliwa ametoa wito kwa Wakazi wa maeneo hayo kushirikiana na Mkandarasi anayejenga daraja hilo ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kumaliza mradi huo kwa wakati.

 

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Ndanda, -  Cecil Mwambe ameipongeza na kuishukuru Serikali kwa jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo pamoja na kubadilisha maisha yao.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment