Responsive image
Responsive image
Posted : July 12, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa mwaka wa Chama cha Kampuni za Simu Duniani jijini Dar es Salaam.
Responsive image

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema  kuwa Serikali itaendelea kusimamia na kuweka mazingira bora yatakayosaidia mamia ya wananchi kupata huduma za mawasiliano ya simu kwa njia ya kisasa zaidi mijini na vijijini.

 

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Chama cha Kampuni za Simu Duniani unaofanyika  Jijini Dar es salaam.

 

Amesema  kuwa ana imani kuwa wadau wa Kampuni  hizo za simu watajadili kwa kina namna bora ya kufikisha mawasiliano ya kisasa kwa wananchi na kuweka mipango mizuri ya kufikia wananchi wengi zaidi hasa maeneo vijijini ambayo baadhi yao hayafikiki kutokana na uduni wa miundombinu.

 

Makamu Samia Suluhu Hassan pia amesisitiza umuhimu wa kuimarishwa zaidi kwa huduma za kisasa za kimtandao ili wananchi waweze kunufaika zaidi kwa njia hiyo katika sekta za elimu, afya, kilimo, biashara na masuala ya kijinsia.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI
Ladies FashionBENEDICTO F.  |  9 months ago   |   July 16, 2017
"Napenda Kupata Habari Moto Moto Kutoka Tbc"

Leave Your Comment