Responsive image
Responsive image
Posted : July 08, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo alipotembelea na kukagua mradi wa awamu ya Pili wa Kufua Umeme wa Gesi Asilia wa KINYEREZI II.
Responsive image

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa awamu ya Pili wa Kufua Umeme wa Gesi Asilia wa KINYEREZI II.

 

Akizungumza jijini Dar es salaam  na wananchi pamoja na  watendaji wakuu wa Shirika la Umeme nchini -TANESCO alipotembelea na kukagua mradi huo,Waziri Mkuu Majaliwa amesema azma ya serikali ni kuimarisha vyanzo vya uzalishaji wa nishati ya umeme ili kuongeza  upatikanaji wake utakaoweza kukidhi mahitaji halisi ya watanzania.

 

Amesema endapo Tanzania itakua katika hali nzuri ya uzalishaji wa nishati ya umeme kuna uwezekano mkubwa wa kukaribisha wawekezaji wengi kuwekeza katika sekta ya viwanda hapa nchini.

 

Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Kufua wa Umeme wa Gesi Asilia  Awamu ya Pili  KINYEREZI II Mhandisi Stephen Manda amesema licha ya kuendelea kukamilisha mradi huo bado kuna changamoto mbalimbali  zikiwemo tozo za kodi ambazo zinawakwamisha utekelezaji wa mradi huo.

 

Kwa sasa Tanzania ni nchi pekee katika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  na Kati ambayo imepiga hatua katika kuendeleza huduma ya uzalishaji wa umeme  ambapo imefikia asilimia 66 ya kuzalisha na kusambaza umeme nchini ikiwa na matarajio ya kufikia Asilimia 100  ifikapo 2018.

 

 

 KULTHUM ALLY

JULY 09 2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment