Responsive image
Responsive image
Posted : July 06, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Responsive image

Timu ya Taifa (Taifa stars) imetolewa kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la COSAFA baada ya kufungwa na timu ya Taifa ya Zambia.

Taifa Stars imefungwa bao nne kwa mbili na timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopolo) ingawa yenyewe ilitangulia kufunga goli la mapema ambalo lilionyesha nyote njema kwa Taifa Stars kabla ya kibao kubadilika.

Erasto Nyoni aliifungia Taifa stars goli la kwanza kwenye dakika ya 14 na Zambia wakasazisha kwenye kipindi hicho hicho cha kwanza na kufunga goli la pili kabla ya mapumziko.

Kwenye kipindi cha pili Zambia ilifunga magoli mengine mawili na Taifa Stars ikafunga goli moja lilofungwa na Simon Msuva na kufanya mchezo huo umalizika kwa ushindi wa Zambia wa bao nne kwa mbili.

 

Huu ni mchezo wa kwanza kupoteza kwa kocha Salum Mayanga tangu apewe jukumu la kuinoa timu hiyo ambapo amecheza michezo nane, ameshinda michezo minne, sare michezo mitatu na kupoteza mchezo mmoja.

 

 

EVANCE MUHANDO

JULY 07 2017

 

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment