Responsive image
Responsive image
Posted : July 04, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Makamu wa Kwanza Rais wa Sudan Kusini Jenerali Taban Deng Gai (kulia) ameoimba Tanzania kuisaidia katika utoaji wa mafunzo kwa wataalamu wake hasa wa sekta ya afya, kilimo na kupatiwa walimu wa lugha la Kiswahili alipokutana na makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu
Responsive image

Serikali ya Sudan Kusini imeoimba Tanzania kuisaidia katika utoaji wa mafunzo kwa wataalamu wake hasa wa sekta ya afya, kilimo na kupatiwa walimu wa lugha la Kiswahili kwa sababu taifa hilo linataka kuanza kufundisha lugha hiyo kwenye shule mbalimbali nchini humo.

 

Makamu wa Kwanza Rais wa Sudan Kusini Jenerali Taban Deng Gai ametoa maombi hayo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kando mwa Mkutano 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

 

Jenerali Taban Deng ameishukuru Tanzania kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Sudan Kusini kupitia Jumuiya mbalimbali hususan Jumuiya ya Afrika Mashariki katika juhudi zake za kutafuta amani ya kudumu na kuwavumilia kadri inavyowezekana hasa wanapopitia changamoto mbalimbali kufikia amani hiyo. 

 

Kwa upande wake, Makamu wa Rais Samia ameihakikishia Sudani Kusini kuwa Tanzania itakuwa mstari wa mbele  kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii ikiwemo juhudi za uimarishaji wa hali ya ulinzi na usalama katika taifa hilo.

 

 

TAARIFA

JULAI 04,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI
Ladies Fashiondeograyius magoma  |  7 months ago   |   August 30, 2017
"huruma xana. "

Leave Your Comment