Responsive image
Responsive image
Posted : July 03, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Elias Maguri akichuana na Mchezaji wa Afrika Kusini katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya COSAFA, 2017, ambapo Taifa Stars ilishinda kwa bao 1-0 na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.
Responsive image

Timu ya Taifa (Taifa Stars) imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la COSAFA baada ya kuilaza timu ya Taifa ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) bao moja kwa bila.

 

Goli pekee la Taifa Stars lililotiwa kimiani na mshambuliaji Elias Maguli kwenye dakika ya kumi na nane ya mchezo huo.

 

Wenyeji Bafana Bafana walimiliki sehemu kubwa ya mchezo huo na waliliandama lango la Taifa Stars karibu kwa muda wote lakini uimara wa ngome ya ulinzi ya Taifa Stars iliyoongozwa na mkongwe Erasto Nyoni ilifanya kazi nzuri na kuondoa hatari zote huku mlinda mlango Aishi Manula akiendelea kuonyesha kuwa hivi sasa yeye ni Tanzania one kwa kuokoa michomo kadhaa.

 

Kwa ushindi huo wa bao moja kwa bila dhidi ya Bafana Bafana sasa Taifa Stars itacheza nusu fainali na timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopolo) siku ya jumatano.

 

 

EVANCE MHANDO

JULAI 03,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment