Responsive image
Responsive image
Posted : July 03, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Tanzania Footbal Federation.
Responsive image

Kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka hapa nchini (TFF) ,imesitisha zoezi la uchaguzi hadi hapo utakapotangazwa tena,baada ya kutokea kutokuelewana kwa wajumbe  wa kamati hiyo.

 

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Revocatus Kuuli,amesema kumetokea mvutano mkali wakati wa kujadili ni mgombea yupi aendelee na mchakato huo wa uchaguzi na nani akatwe kutokana na matokeo ya Usaili huku kaimu katibu mkuu wa TFF Salum Madadi akisema,kamati ya utendaji ya TFF itafanya kikao cha dharura siku ya Jumanne kujadili sakata hilo la uchaguzi.

 

Wakati zoezi hilo la uchaguzi waTFF,likisitishwa,siku ya Jumatatu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itatoa uamuzi wa kesi inayowakabili,Rais wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi na Katibu wake, Mwesigwa Selestine wanaokabiliwa na tuhuma 28 ikiwemo tuhuma za kutakatisha fedha.

 

 

 

EVANCE MHANDO

JULAI 03,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment