Responsive image
Responsive image
Posted : July 03, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Mabingwa wa kombe la mabara 2017, Ujerumani
Responsive image

Mabingwa wa dunia timu ya Taifa ya Ujerumani imetwaa kwa mara ya kwanza ubingwa wa kombe la mabara baada ya kuilaza Chile bao moja kwa bila.

 

Goli pekee la Ujerumani lilitiwa kimiani na Lars Stindl kuafutia uzembe uliofanywa na  mlinzi wa kati wa Chile Marcelo Diaz.

 

Chile waliliandama mno Ujerumani lakini walishindwa kupata bao kufuati ngome imara ya Ujemani ambayo iliundwa na wachezaji wengi chipikizi.

 

Michuano ya kombe la mabara hufanyika mwaka mmoja kabla ya michuano ya kombe la Dunia na nchi mwenyewe wa michuano ya kombe la Dunia ndio huwa mwenyeji wa michuano ya kombe la Mabara na  ndio maana Russia wameanda michuano ambao  pia watakuwa wenyeji wa kombe la Dunia la  mwakani 2018.

 

 

EVANCE MHANDO

JULAI 03,2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment